Wakati BASATA
wakimtuhumu Diamond kulewa na umaarufu na kufanya abishae na Naibu waziri
ambaye anawakilisha Serikali, bado huko katika mitandao ya kijamii watu
wamezidi kuonyesha hisia zao juu ya jambo hilo kwa kudai kuwa Naibu waziri
anatafuta kiki kwa lengo la Kumshusha Diamond.
Mwanahabari na
Blogger, Le Mutuz ameibuka na kudai kwa Naibu Waziri amekuwa akitumiwa na watu
wenye chuki kubwa na muziki wa Diamond ili kuua muziki wake na sio vinginevyo.
Le Mutuz anasema
kuwa huu ulikuwa ni wakati wa serikali kuona mchango wa Diamond hasa
baada ya kuchaguliwa kwenda kufanya show ya ufumbuzi wa kombe la
Dunia.
Hata hivyo Lemutuz
amemhusisha Julana Shonza na moja ya kiongozi wa kituo fulani cha radio “MUNGU
MTU” ambacho hajakitaja na kusema kuwa wamekuwa wakishirikiana ili kumtua
Diamond katika nafasi kubwa ya mafanikio ya kimuziki aliyonayo.
Lemutuz Amkingia Kifua Diamond....Amtuhumu Naibu Waziri Kushirikiana na Watu Kumshusha Diamond
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment