Balozi wa Tanzania
nchini Rwanda, IGP Mstaafu Ernest Mangu amemuahidi Rais Dkt. Magufuli kwamba
atahakikisha anadumisha mahusiano mazuri baina ya Rwanda na Tanzania ili kuweza
kuipeleka nchi katika maendeleo mazuri ya kiuchumi.
Balozi Mangu ametoa kauli hiyo
wakati alipokuwa anatoa salamu zake kwa Rais Magufuli pamoja na viongozi
wengine walihudhuria hafla hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam ya kula kiapo cha
Utii ili kuweza kutumika nafasi aliyoteuliwa.
"Nimefarijika sana kuona Rais
Magufuli bado unaendelea kunikumbuka na kuona bado naendelea kufaa kutumika
chini yako. Ninachokuahidi kwamba nitaendelea kuwa muaminifu, ntatumia nguvu na
akili zangu zote kuhakikisha kwamba natekereza majukumu ya kibalozi kama
ambavyo yameanishwa kwenye sheria na taratibu mbalimbali", amesema Balozi Mangu.
Pamoja na hayo, Balozi Ernest Mangu
ameendelea kwa kusema "naelewa umuhimu wa nchi ya Rwanda kwa
maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na hasa katika sekta ya bandari, usafirishaji
na masuala mazima ya uhusiano ya kimataifa hivyo naahidi nitaenda kufuatilia
mambo yote hayo ili kuweza kudumisha uhusiano wetu na nchi za jirani".
Kwa upande mwingine, Makamu wa Rais
Samia Suluhu amempongeza Balozi Ernest Mangu wa Tanzania nchini Rwanda, na Meja
Jenerali Mstaafu Simon Marco Mumwi wa Urusi kwa kuweza kula kiapo siku ya leo
(Machi 21, 2018) na kuwataka wakabiliane na kazi nzito iliyokuwa mbele yao ili
kuweza kuileta matunda mazuri nchi yao Tanzania kwa kile watakachokifanya huko.
Balozi Mangu aahidi mazito kwa JPM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment