Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa
imezuia dhamana ya Mwenyekiti wa Mtandao Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo
kwa sababu za usalama wake ikieleza kuwa bado maisha yake yapo hatarini.
Akizungumza leo Jumatano Machi 21, 2018
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, John Mpitanjia amesema anaomba muda wa kusoma
vifungu vya sheria mpaka Machi 26, 2018 ili kujihakikishia kama mtuhumiwa
hatakuwa hatarini iwapo atapatiwa dhamana
Akisoma mashkata yanayomkabili Nondo, Wakili
wa Serikali, Abeid Mwandalamo amesema anatuhumiwa kwa makosa mawili
Amesema kosa la kwanza ni kuchapisha
taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa eneo la Ubungo Dar es Salaam na
kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.
Katika shtaka la pili, wakili huyo amesema
Nondo ametoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa
anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi Mafinga kwa kusema kuwa
alitekwa na watu wasiojulikana Dar es Salaam na kupelekwa kiwanda cha Pareto
Mafinga. Hata hivyo, Nondo alikana mashtaka hayo.
Mwanadalamo amesema ushahidi bado
haujakamilika hivyo wanaomba siku chache, kwa kipindi watakachokuwa wanafanya
upelelezi mtuhumiwa asipewe dhamana.
Amedai kuwa kwa sababu bado wanafanya
upelelezi kwa rafiki wake wa karibu, kama atapewa dhamana anaweza kuingilia na
kuharibu upelelezi huo.
Wakili wa utetezi, Chance Luwoga amesema
mashtaka aliyosomewa Nondo yanaruhusu kupewa dhamana.
Nondo asomewa mashtaka mawili, anyimwa dhamana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment