Kikongwe wa miaka 90 adaiwa kubaka watoto watano

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia mzee mwenye umri wa miaka 90, Kachuka Malongo kwa tuhuma za kubaka wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Tinde, Wilaya ya Shinyanga

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule alisema kwamba wanafunzi hao walibakwa kwa nyakati tofauti na mtuhumiwa akiwarubuni kwa kuwapa pipi na pesa

“Tumebaini chanzo cha tukio hilo kuwa ni tamaa na uchu wa mapenzi. Tayari tunamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani,” alisema Kamanda Haule

Akizungumzia tukio hilo Kamanda Haule alisema kwamba mkazi wa Tinde, Amada Mganyizi ndiye aliyebaini kubakwa kwa wanafunzi hao Machi 21 saa 2:30 asubuhi. Hata hivyo, hakueleza kwa undani namna gani mkazi huyo alibaini kubakwa kwa watoto hao.

Alisema kwamba wanafunzi hao ambao majina yao yanahifadhiwa wana umri wa kati ya miaka minane na 12 na wanasoma katika shule za msingi Tinde A na B.
“Natoa rai kwa wananchi na wazazi kuwa makini na karibu na watoto wao ili kubaini mabadiliko yao. Lakini kitu kingine kikubwa, nawataka wachukue hatua za haraka wanapobaini watoto wamefanyiwa ukatili kama huu,” alisema
Kamanda huyo.Aliwaonya watu wazima wenye  tabia hizo kuacha mara moja.Baadhi ya wananchi wa Tinde A waliohojiwa kuhusu tukio hilo walisema endapo itabainika kwamba ni kweli kwamba mzee huyo amefanya hayo, achilia mbali kuwa kitakuwa ni kitendo cha ukatili, pia kitakuwa ni cha aibu kufanywa na mzee wa umri huo
Hussein Seif alisema wamesikitishwa na taarifa za mzee huyo kuhusishwa na kitendo cha kubaka wajukuu wake

Joseph Kija alisema wanaofanya vitendo hivyo wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo
Kikongwe wa miaka 90 adaiwa kubaka watoto watano Kikongwe wa miaka 90 adaiwa kubaka watoto watano Reviewed by KUSAGANEWS on March 25, 2018 Rating: 5

No comments: