|
|||
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kupitia kamati
yake ya utekelezaji ya baraza kuu umepitisha vipaumbele vyake vinne kwa
mwaka 2018/20.
Akizungumza mwenyekiti wa
umoja huo, Gaudensia Kabaka amesema kikao hicho kimekubaliana kuanza na
vipaumbele hivyo vinne.
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kufuatilia
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015/2020, kwa kuungana na
Serikali kupitia idara ya maendeleo ya jamii kuanzia kata mpaka Taifa.
Wajibu wetu utakuwa kuhoji na kufuatilia huduma za
jamii kama maji, elimu, afya ya mama na mtoto, lengo ni kuhakikisha kila
kilichomo ndani ya ilani kinafanyiwa kazi kama kilivyoainishwa, ” amesema
Kabaka.
Amesema kipaumbele cha pili ni kujiimarisha kiuchumi
kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuendeleza vyanzo vilivyopo kuanzia
ngazi ya kata mpaka Taifa
“Vipo vyanzo vingi vya mapato ambavyo UWT haijaviibua,
tunajipanga upya kuanza kujipambanua ili kuwa na tija katika jamii,” amesema
“UWT si masikini, tuna mashamba, majumba na viwanja.
Tumefanya tathmini ya kuvitambua kwanza katika mikoa ya Arusha na Dar es
Salaam, tunaendelea katika mikoa mingine, ili tujiendeshe kwa tija zaidi
Amesema kipaumbele kingine ni kuongeza wanachama
kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa, “UWT kama chombo cha kisiasa lengo lake pia
ni kushika dola, hivyo wanachama hawa wapya ni mtaji wa uchaguzi hasa
tunapoelekea chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu 2020,”
amesema Kabaka
Amesema jambo lingine watakaloliangazia kwa karibu ni
kuwajengea uwezo viongozi, watendaji, wanachama, vikundi vya wanawake vya
uchumi na kijamii wakiwamo watoto katika masuala mbalimbali
“Tutatoa mafunzo ya mbinu za uongozi nchi nzima na
tayari tumeshajipanga kwa hilo, uchumi na ujasiriamali, mapambano dhidi ya
rushwa na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto,”
amesema
“Vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni
suala linaloninyima raha, hata nikiiona habari yake gazetini au kwingineko
huwa nashindwa kumaliza kuisoma kwa sababu inauma sana.”
|
|||
|
|||
|
|||
JUMUIYA YA WANAWAKE UWT YAPITISHA VIPAU MBELE VINNE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment