Watu wawili wamefariki dunia na nyumba
sita zikiezuliwa na upepo wilayani Handeni mkoani Tanga kutokana na mvua kubwa
iliyonyesha jana, Machi 9, jioni.
Akielezea tukio hilo Diwani wa kata ya Msasa wilayani hapa Hossein Omari amesema mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Mhando (32) amefariki baada ya kupigwa na radi wakati akitoka msikitini saa kumi jioni.
Amesema shuhuda wa tukio hilo, aliyekuwa akitoka na marehemu msikitini aliwaeleza kuwa mvua wakati inanyesha alisikia mlio wa radi na baadae kuona mwenzie anatoka moshi na kubaini amepigwa na radi.
Ndugu wanasema mwili hauna jeraha lolote ila nguo ndio zimeungua na radi huku mwili kuonekana kuwa mweusi ila hana majeraha baada ya kupigwa na radi hiyo,”alisema Diwani Hossein.
Amesema wanaendelea kufuatilia kama kuna
madhara zaidi na baadae watatoa taarifa kamili ya madhara yaliyotokea kwa
vyombo husika.
Katika tukio jingine,mkazi wa kijiji cha
Zavuza kata ya Kiva wilayani hapa Mwanahawa Ngoma(60) amefariki dunia baada ya
kusombwa na maji wakati akitoka shambani kulima.
Akizungumzia madhara hayo Mtendaji wa kijiji
hicho Rahma Bakari amesema walipata taarifa ya mtu kusombwa na maji na
kutafutwa usiku mzima ila mwili ulionekana siku ya leo Machi 10.
Ameongeza pia nyumba sita katika kijiji
hicho zimeezuliwa na upepo na kuwaacha wakazi wa eneo hilo bila makazi kutokana
na kunyesha mvua iliyoambatana na upepo Ijumaa jioni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Edward
Bukombe amesema hana taarifa za matukio hayo na akaahidi kufuatilia na
kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua hizo
WAWILI WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment