Kamishna wa Operesheni
na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Nsatu Marijan amesema hali ya usalama nchini
imezidi kuimarika kwani hakuna tishio lolote la kiuhalifu linaloweza kutokea
kwasababu Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo na halishindwi na chochote.
Kamishna Marijan ametoa kauli hiyo
wakati alipokuwa anatoa salamu za kumuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
(IGP), Simon Sirro katika uzinduzi wa vituo vidogo vya polisi vinavyo hamishika
'mobile Police Station' ambapo vitaanza kutumika katika mkoa wa kipolisi
Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
"Jeshi liko imara, matukio ya
uhalifu nchini yamepungua sana, hakuta tishio lolote ambalo lipo nje ya uwezo
wa Jeshi la Polisi kushindwa kulikabiri. Sisi kama Jeshi la Polisi tutaendelea
kuhakikishia nchi hii inaendelea kuwa salama ili wawekezaji na wananchi waweze
kufanya shughuli zao bila ya taflani yeyote", amesema Kamishna Marijan.
Pamoja na hayo, Kamishna Marijan
ameendelea kwa kusema "kama mtu ana wasiwasi na Jeshi letu basi
ajaribu kufanya lolote maana wanasema asiyejua kufa basi akachungulie kaburi.
Sisi tupo imara tutaendelea kuwa imara".
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema vituo hivyo vilivyo
zinduliwa leo vitatumika kwa kadri ya maelekezo ya maeneo yenye uhalifu
utakapotokea eneo fulani na endapo utapungua basi watavihamishia na kwenda eneo
jingine lenye uhalifu.
Hakuna Tishio lolote la Kiuhalifu - Jeshi la Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment