Msanii mkongwe wa
BongoFleva nchini Afande sele atangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi
(CCM) leo mbele ya Rais Dkt. Magufuli kwa lengo la kuunga mkono jitihada zake
anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama kimpokee kama kijana wao.
Afande Sele ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa anatumbuiza muziki kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro walioweza
kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha Sigara mkoani humo na Rais
Magufuli.
"Nataka nimuhakikishie Mhe.
Rais Dkt. John Magufuli kwamba mimi ni mtu wakufikiri, mbishi na mgumu sana
katika kukubali jambo fulani lakini niseme kwa uwazi kabisa tangu ulipochukua
madaraka ya kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM umeweza kuinyosha nchi na
kukisafisha chama chako na kimeweza kurudi katika uhimara wake kama alivyokuwa
anataka muasisi wetu wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere lakini leo kimekuwa
hivyo", amesema Afande Sele.
Pamoja na hayo, Afande sele
ameendelea kwa kusema "naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini
kama haitoshi naomba nikuhakikishie kwamba leo hii kutoka kwa dhati ya moyo
wangu nimeamua nisimame upande mmoja na wewe ili nisiachwe katika maendeleo.
Ninaamini kabisa Mhe. Rais sasa hivi Tanzania kama gari basi dereva ametulia na
gari linakwenda na mimi kama abiria niachwe ninywe soda yangu kwa amani
kwasababu naamini kabisa chombo chetu kinaenda sehemu salama na sipendi kesho
historia ije kunihukumu kwa watu wale ambao hawakuchangia walichonacho katika
kufikisha mahali kinapoenda".
"Nawaomba viongozi ngazi ya
mkoa wa CCM mnipokee kijana wenu nije kuongeza nguvu", amesisitiza Afande sele.
Kwa upande mwingine, Afande
Sele aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Morogoro Mjini mwaka 2015 kupitia chama
cha ACT Wazalendo kabla ya kujivua uanachama na kusema kuwa hataki tena
kujihusisha na siasa.
AFANDE SELE AHAMIA CCM LEO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment