Ofisa Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Joyce Amon amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka
la kushawishi rushwa
Wakili wa Serikali, Sophia Nyanda amesema leo Ijumaa Machi
9, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore
kuwa Desemba 12, 2017 katika eneo la Gerezani Kariakoo
Wilaya ya Ilala mshtakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa TRA kama Ofisa Msaidizi wa
Kodi alishawishi rushwa ya Sh800,000 kutoka kwa Antelo Sanga ili asiweze
kumwandikia cheti cha faini cha Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT).
Katika shtaka la pili,
mwanafunzi Lilian Wilson (23) naye anakabiliwa na
shtaka la kusaidia kutenda kosa hilo.
Wakili Nyanda amedai Desemba 13,2017 katika Hoteli ya
Tansome mshtakiwa huyo Lilian alimsaidia Joyce ambaye ni Ofisa
Msaidizi wa Kodi wa TRA kujipatia Sh400,000 kutoka kwa
Antelo Sanga ili asiweze kumpatia cheti cha faini
cha VAT
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa walikana na
upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hakimu Sachore alimtaka kila mshtakiwa kuwa na
wadhamini wawili wenye barua kutoka katika taasisi zinazotambulika
kisheria ambao watasaini ahadi ya Sh5 milioni kwa kila mmoja. Na
kwamba barua hizo zitahakikiwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20, 2018 kwa ajili ya
kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.
Apandishwa kizimbani kwa kushawishi rushwa ya Shilingi 800,000
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment