Mtoto aliyeokolewa kwenye ajali ya meli ya MV Bukoba mwaka 1996 akiwa na
umri wa miaka minne, Samuel Paschal anatarajia kuachia albamu yake ya video
katika uzinduzi utakaofanyika April 22, 2018 mkoani Arusha.
Samuel aliokolewa kwenye ajali hiyo lakini
wazazi wake wote wawili walipoteza maisha
Akizungumza kwa njia ya simu Samuel ambaye
kazi zake tayari ameziachia katika akaunti yake ya ‘Youtube’amesema uzinduzi
huo utaambatana na shukrani zake kwa Mungu kwa kuweza kufikia hatua hiyo
"Natamani kumshukuru Mungu sana kwa
kunifikisha hapa na uhai nilio nao na nachoomba ni sapoti ya Watanzania
wenzangu kwenye kazi hii ya kipaji niliyoamua kuifanya," amesema
Muimbaji huyo wa muziki wa injili ambaye pia
kuna nyimbo amemshirikisha Tumaini Martin au Matumaini wa Kiwewe, amesema
uzinduzi wake utafanyika katika Kanisa la KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati,
Usharika wa Sokoni Ngulelo
Nani anifute Machozi ndilo jina la albamu
yangu iliyosheheni video kali ambazo naamini kila atakayezipata atakubali tena
kukata tamaa hata kama kuna jambo gumu linalomzunguka,” amesema
Amesema waimbaji lukuki wanatarajia
kumsindikiza katika uzinduzi huo akiwamo Angel Bernard.
Aliyenusurika ajali MV Bukoba kuzindua album nyimbo za injili
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment