Vilio, simanzi na kupoteza fahamu
kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa
mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.
Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa
leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.
Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa
akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza
lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza
na Shirika la Msalaba Mwekundu
Viongozi waliofika mpaka sasa
katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk
Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Lazaro Mambosasa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.
Tayari ibada ya kuaga mwili wa
mwanafunzi huyo imeanza.
|
|
Wanafunzi wapoteza fahamu baada ya kuona jeneza la Akwilina
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 22, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment