Mahakama ya jijini Cairo nchini Misri imewahukumu kifo watu 21 kwa
kosa la kujihusisha na ugaidi kwa nyakati tofauti.
Watu hao walikutwa na hatia ya kujiunga na makundi ya kigaidi na
kupanga mashambulizi dhidi ya watu wasio na hatia, majengo ya sekta binafsi na
sekta ya umma. Wanadaiwa pia kupanga kuwaua askari wa jeshi la polisi na jeshi
linalolinda mipaka ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Misri, watu hao wanadaiwa pia
kupanga kufanya mashambulizi ya mabomu katika vituo vya polisi katika Pwani ya
jiji la Damietta pamoja na bomba la gesi katika kijiji cha jirani.
Hukumu ya mwisho ilipitishwa na mahakama ya nchi hiyo na baadaye
kupitishwa na kiongozi mkuu wa kidini nchini humo (Grand Mufti), Sheikh Shawki
Allam.
Baadhi ya watuhumiwa hawakuwa mahakamani wakati hukumu dhidi yao
ilipokuwa inasomwa.
21 wahukumiwa kifo, kiongozi wa dini abariki
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 22, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment