Njombe, kufuatia kusambaa kwa taarifa inayosemekana kuwa kundi
kubwa la Askari polisi kuvamia nyumbani kwa mwandishi wa habari usiku wa manane
na kumkamata mwandishi huyo Emmanuel Kibiki wa Gazeti la Raia Mwema.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu amekanusha
madai hayo na kusema wao hawahusiki na kukamatwa kwa mwandishi huyo na kudai
huenda akawa amekamatwa na taasisi nyingine ila si jeshi la polisi.
”Hakuna ukweli wowote ule kama kungekuwa na ukweli stori
ingekuwa imeshafika kwetu ila inawezekana labda taasisi zingine za upelelezi
zinafanya kazi zikawa zimemkamata maana taasisi za upepelezi huwa zinawakamata
watu zenyewe, kwa hiyo watu wanapicha tu kuwa mtu akikamatwa basi jeshi la
polisi ndilo linakuwa limemkamata.
Kwa sababu kama sisi tungekuwa tumemkamata mpaka asubuhi hao
polisi wangekuwa wamewasiliana na mkoa kutoa taarifa” amesema Temu
Aidha kwa mujibu wa taarifa za awali zinasemekana kuwa mwandishi
huyo alivamiwa na askari ambao idadi yao haikujulikana na kulazimisha
kuingia ndani kufanya upekuzi na kumkamata kwa kosa la kuandika habari za
siasa.
”kosa lake ni kwamba anaandika sana mambo ya siasa na
waliowatuma hawapendi.
Wamemchukua tangu saa tisa usiku na hajarejea mpaka muda huu,”
Tobina ambaye ni mke wa mwandishi huyo amenieleza kwa kilio cha kwikwi muda
mchache uliopita” amesema Ezekiel Kamwaga amabaye ni mhariri wa Gazeti la Raia
Mwema.
Emmanuel Kibiki amekuwa akifanya kazi mjini Makambako, Njombe na
amekuwa akiandika mawazo yake katika mitandao ya kijamii na magazeti mbalimbali
likiwamo Raia Mwema.
Polisi yakana kuhusika kukamatwa kwa mwandishi wa habari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 22, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment