Chadema
kimetoa sababu za viongozi wake wakuu watatu akiwamo Freeman Mbowe
zilizowafanya wasiitikie wito wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Mbowe pamoja
na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji na Naibu Katibu Mkuu wa Chama
hicho-Zanzibar, Salum Mwalimu ni kati ya viongozi saba wa Chadema waliopaswa
kufika Kituo Kikuu cha Polisi leo Februari 20 lakini hawakufika
Akizungumza
leo Februari 20, 2018 Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa
Chadema, John Mrema amesema wakati wanapokea barua ya wito wa polisi kwa
viongozi hao kufika kituoni wengine walikuwa wametawanyika
“Mfano, Salum
Mwalimu jana alitangulia Mafinga (Iringa) kwa ajili ya kuongoza mazishi ya
kiongozi wetu Daniel John hivyo kwa wito tulipokea asingeweza kufika sawa na
Mwenyekiti (Mbowe) alikuwa nje ya Dar es Salaam,” amesema Mrema na kuongeza
“Katibu Mkuu
(Dk Mashinji) wakati tunapokea wito yeye alikuwa safarini kwenda Marekani kikazi
na alisafiri saa 10 jioni akipita ‘airport’ ya Dar es Salaam, kwa hiyo kama
wangetoa taarifa mapema wangeweza wao wenye kumdaka pale pale ‘airport.”
Mrema amesema
viongozi hao watakaporejea kabla ya Jumanne ya Februari 27, 2018 wanayotakiwa
kuripoti na viongozi wengine watakwenda kuitikia wito huo.
Viongozi
walioripoti leo kituoni hapo na kuachiwa kwa dhamana ni, Naibu Katibu Mkuu-
Bara, John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha),
Halima Mdee, Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Ester Matiko
ambaye ni Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Bawacha.
SABABU YA MBOWE KUTOFIKA POLISI LEO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 20, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment