Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hakuna sababu ya
wakandarasi wa miradi ya maji kuagiza mabomba nje ya nchi wakati kuna mabomba
yanayozalishwa hapa nchi tena kwa ubora hivyo kuwataka watumie ya ndani
Ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda
cha kuzalisha mabomba cha Mwanza Plastics eneo la Nyamhongolo wilayn Ilemela
Mwanza.
Niwatake wakandarasi tuendelee kutumia mabomba ya ndani ili
kuendelea kutoa sapoti kwa wawekezaji hawa,"amesema
Kwa kusimamia hilo ameagiza miradi yote ya maji
inayotekelezwa katika halamshauri za mkoa huo kuhakikisha mabomba ya maji
yananunuliwa katika kiwanda hicho cha mzawa ilmradi kiwango cha mabomba hayo
yawe yanapatikana hapo
"Kuna mradi wa kusambaza maji katikati ya mji wa Sh14
bilion ambao upo hatua za manunuzi, mkurugenzi wa Mwauwasa simamia hilo
wakandarasi wanunue mabomba kiwanda hiki," amesema Waziri
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho John Charles alisema
kiwanda hicho chenye wafanyakazi 15 wazawa wenye ajira za kudumu na watatu
kutoka nje ya nchi, kilianza mwaka 2008 kwa kutengeneza plastiki na vikombe.
Amesema wanakabiliwa na uhaba wa umeme wa kutosha kwani
unakuwa wakati mwingine unakosa nguvu na miundombinu ya barabara hivyo kuonheza
gharama za uzalishaji
Kutokana na hayo waziri alimwagiza mkurugenzi wa manispaa ya
Ilemela John Wanga kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji kuhakikisha
miundiombinu yote muhimmu inafika.
Majaliwa Hakuna sababu ya wakandarasi kununua mabomba nje ya nchi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 20, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment