Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amesema kuwa muda ukifika itajulikana kama atagombea nafasi ya ubunge kwani hata yeye ana haki ya kikatiba kugombea nafasi hiyo.
Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza amesema kuwa kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia suala hilo, hivyo anachokifanya kwasasa ni kutoa huduma mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji.
Amesema kuwa Mbeya ni nyumbani hivyo kufanya shughuli nyingi za kijamii mkoani humo si kwamba anatafuta nafasi ya kugombea ubunge ingawa ana haki ya kufanya hivyo.
“Ni haki yangu kikatiba kugombea na muda ukifika watu watajua tu, lakini kwasasa siwezi kusema chochote kuhusu kugombea ubunge,”amesema Dkt. Tulia
Naibu Spika adai nina haki ya kikatiba kugombea ubunge
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 20, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment