Mbunge mteule wa jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro Dokta
Godwin Mollel Amekubaliana na wananchi wake fedha kiasi cha Milioni 13 alizokuwa
ametenga kwa ajili ya kufanya sherehe ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge zielekezwe katika miradi
ya Elimu na afya.
Baada ya Dokta Mollel Kuchaguliwa katika Februari 17
alifanya ziara kwenye kata tofauti tofauti kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa
kumchagua wakafanya makubaliano hayo ambapo sasa fedha hizo zinakwenda
kutekelezawalichokubaliana na wananchi.
Akizungumza na Kusaga News Mollel amesema kuwa kwasasa
jambo lililopo n kuchapa kazi kwasababu porojo zimeisha na wananchi walikuwa
wanataka maendeleo ambayo yeye kwa kushirikiana na wananchi wake ameahidi
atatekeleza.
“Kweli Ndugu mwandishi baada ya ushindi wa tarehe 17
nilipata nafasi ya kupita kwene kata tano tofauti ,Ngarenairobi,Sanya
Juu,Nasai,na kirua na wananchi kwa kweli wananchi tumekubaliana fedha zotehizo za
sherehe milioni 13 tuelekeze katika elimu na afya kwa kuwa wao ni wapenda
maendeleo namimi ni mbunge wao niliye ahidi kwatumikia”Alisema Mollel
Hata hivyo katika kushurukuru wananchi kwenye kata ya Karansi
amechangia wananchi milioni 2 ilikumalizia darasa moja badala y kufanya
sherehe.
Mbunge wa jimbo la Siha alichaguliwa tarehe 17 mwezi
februari baada ya kurudiwa kwa uchaguzi uliotokana na Mbunge Dokta mollel
aliyejiuzulu Chadema na kujiunga na Ccm na kugombea tena na kuchaguliwa na
wananchi
MILIONI 13 ZA SHEREHE ZAELEKEZWA KWENYE MIRADI YA ELIMU NA AFYA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 20, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment