Ratiba ya kuaga mwili wa Akwilina Akwiline, mwanafunzi wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) aliyefariki dunia kwa kupigwa risasi
Februari 16,2018 itaanza saa tatu asubuhi Alhamisi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 20,2018
nyumbani kwa dada wa Akwilina, baba mdogo wa marehemu Valentino Akwiline
amesema wanatarajia kuusafirisha mwili Alhamisi Februari 22,2018 kuelekea
Mashati Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika
Ijumaa
Amesema ratiba itaanza saa tatu asubuhi kwa mwili kufikishwa
nyumbani kwa Tegolena Uiso ambaye ni dada wa Akwilina ambako kutafanyika ibada
"Mwili utaondoka Muhimbili saa tatu asubuhi kuja hapa
nyumbani, tunatarajia ufike saa tano asubuhi na kutakuwa na misa fupi na
chakula kwa watakaohudhuria.”
"Tunatarajia saa saba mwili utaondoka hapa nyumbani
kuelekea katika viwanja vya Chuo cha NIT ambako shughuli kubwa ya kuaga mwili
zitafanyika. Saa tisa alasiri tutaanza safari kuelekea Rombo," amesema
Familia yatoa ratiba ya kuaga mwili wa Akwilina
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 20, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment