POLEPOLE AFURAHISHWA NA HALMASHAURI YA JIJI JINSI WALIVYOJIPANGA KUSAIDIA KAYA MASKINI KUPITIA TASAF


Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi taifa Humprey Polepole leo amekagua na kutembelea miradi ya kupunguza umasikini katika jiji la Arusha (TASAF) awamu ya tatu inayogharimu zaidi ya shilingi billion mbili na millioni miatatu arobaini na moja.

Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati akitembelea  miradi hiyo Polepole amesema mpaka  kufikia mwaka 2020/2025 serikali kupitia miradi ya TASAF inatarajia kuwakwamua watanzania zaidi ya asilimia 50 walipo katika Kaya Duni kwa kuwaondoa katika umasikini na kuishi maisha bora zaidi.

Amesema anataka fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya Kaya Masikini zilete tija kwa wananchi ili Tifa liweze kuondokana na umasikini na kufikia katika uchumi wakati ifikapo mwaka 2025; kama ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyoelekeza.

Polepole ameongeza kuwa jiji la Arusha linapaswa kuigwa jinsi wanavyoendesha mchakato wa kusaidia kaya maskini kwa kuwa fedha zinazotolewa na serikali zinawaendea walengwa moja kwa moja na zimewasaidia vizuri tofauti na sehemu nyingine wanavyofanya.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Juma Kihamia ameeleza kuwa jiji la Arusha ni miongoni mwa Halmashauri zinazofanya uhawilishaji wa fedha kwa Kaya Masikini katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo wameweza kutoa fedha kwa kaya 4,184, vyerehani 30, ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu, matundu ya vyoo, na kivuko cha miguu mtaa wa Oloresho.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia amesema mratibu wa TASAF jiji la Arusha Bi. Tajiel Mahega anaendana na kasi ya serikali ya awamu ya TANO kiutendaji 

Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameishukuru serikali kwa kuwaletea mpango huo kwani imewasaidia kujikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao ya kila siku, ambapo wamesaidika katika kupata milo mitatu kwa siku, watoto kwenda shule, pamoja na kufanya biashara mbalimbali zinazowaingizia kipato.

POLEPOLE AFURAHISHWA NA HALMASHAURI YA JIJI JINSI WALIVYOJIPANGA KUSAIDIA KAYA MASKINI KUPITIA TASAF POLEPOLE AFURAHISHWA NA HALMASHAURI YA JIJI JINSI WALIVYOJIPANGA KUSAIDIA KAYA MASKINI KUPITIA TASAF Reviewed by KUSAGANEWS on February 21, 2018 Rating: 5

No comments: