Jeshi la Polisi Mwanza
kushirikiana na TAKUKURU wamemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Misungwi Anthony Bahebe na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Alphonce Sebukoto
kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za umma
Akizungumza na waandishi wa habari,
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kukamatwa kwa
viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na
matumizi mabaya ya madaraka.
Aidha, Kamanda Msangi amesema Bw.
Sebukoto alikamatwa mnamo Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na
wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.
Kwa upande wake, Kamanda wa Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) wa mkoa wa Mwanza Mhandisi
Ernest Makale amesema Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe
katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bahebe.
"Sebukoto aliidhinisha malipo
hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa ana kaimu nafasi ya
Ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa
katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. Kiasi kingine cha fedha
kinachunguzwa kubaini kilipo", amesema
Mhandisi Ernest.
Mnamo Februari 19, 2019 Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi alimsimamisha kazi
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza
achungunzwe na vyombo husika baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza
majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri
hiyo na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.
MWANASHERIA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment