Mwanafunzi mmoja wa darasa la sita wa Shule
ya Msingi Kibohehe, iliyoko wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, amefariki
dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya kuangukiwa na ukuta.
Mwanafunzi huyo wa kiume ameangukiwa na
ukuta wa chumba chadarasa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na
upepo kunyesha leo mchana
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya Simu,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah, amesema mwanafunzi
huyo alikuwa akiingia kwenye kipindi cha dini na ndipo alipokutana
na ajali hiyo ya ukuta na kupoteza maisha
“Mvua ilinyesha na upepo mkali, jengo moja
la darasa likadondoka na kumwangukia mtoto huyo ambaye alikuwa
akiingia kwenye kipindi cha dini,”amesema Issah
Aidha Kamanda amesema, majeruhi wamepelekwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Hai kwa ajili ya matibabu na kwamba
uchunguzi zaidi wa tukio hilo
Mvua yaua mwanafunzi Kibohehe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment