Mtoto wa miaka sita amefariki dunia akiombewa mlimani alikopelekwa
kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumzia
tukio hilo amesema lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima
Gambiwe.
Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa
(25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga
Kamanda amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani
Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye
mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.
MTOTO WA MIAKA SITA AFARIKI AKIOMBEWA KUTOA MAPEPO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment