Mtanzania akamatwa Kenya na dhahabu ya Shilingi Bilioni 2

Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) imekamata dhahabu yenye thamani ya Ksh100 milioni (takriban Sh2 bilioni za Tanzania) na inamshikilia Mtanzania anayehusika na mzigo huo.

Katika taarifa yake, KRA imesema imekamata gramu 32,255.50 za dhahabu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA

Taarifa hiyo imesema, Mtanzania huyo mwenye miaka 46 alikuwa na ankra inayoonyesha mzigo huo una thamani ya dola 859,890 za Marekani
"Mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupata taarifa za kiintelijensia. Alifika Uwanja wa JKIA Ijumaa Februari 16, 2018 akisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision kutoka Mwanza kupitia Kilimanjaro na alikuwa akienda Dubai kwa ndege ya shirika la Kenya Airways," taarifa ya mamlaka hiyo imesema.
Timu ya maofisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ikiongozana na maofisa wa huduma za udhibiti wa mapato walichukua maelezo kutoka kwa mtuhumiwa
"Usafirishaji wa bidhaa ni kinyume cha vifungu vya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya mwaka 2004 sehemu ya 85 (3) na Sura ya Pili ya sehemu B (4) katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki," imesema KRA.
Kifungu hicho cha sheria hakiruhusu usafirishaji wa madini yasiyoongezwa thamani na vito katika ukanda wa Afrika Mashariki

Hivi sasa dhahabu iliyokamatwa iko chini ya KRA, huku maofisa wa forodha na udhibiti wa mipaka wakiendelea na uchunguzi.
Mtanzania akamatwa Kenya na dhahabu ya Shilingi Bilioni 2 Mtanzania akamatwa Kenya na dhahabu ya Shilingi Bilioni 2 Reviewed by KUSAGANEWS on February 21, 2018 Rating: 5

No comments: