Wanachama 400 na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Bagara na Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Ngarenaro Mjini Babati mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi
(Chadema) aliyejiuzulu hivi karibuni wamekabidhiwa kadi za CCM
Katibu wa Uenezi, Siasa, Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga alikabidhi kadi ya CCM kwa wanachama hao wapya na diwani huyo
aliyejiuzulu jana mjini Babati
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi kadi hizo mpya, Lubinga
amewataka wanachama hao 400 na Tlaghasi, kuwa waaminifu kwenye chama hicho.
Amesema CCM ya hivi sasa inaendana na kasi kulingana na dunia
ilivyo, hivyo wajiandae kwenda mwendo kasi ili kufikia maendeleo chanya
Amesema inapotajwa CCM mpya na Tanzania mpya maana yake ni kuwa
Watanzania wa sasa mahitaji yao si ya juzi na jana hivyo viongozi waliopatiwa
dhamana ya kuongoza inawabidi watimize wajibu wao ipasavyo
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM, Tlaghasi amesema amechoka kuishi maisha ya wasiwasi yasiyo na amani, ambayo alikuwa anayaishi wakati akiwa kiongozi wa jamii kupitia Chadema.
Amesema alikuwa anaishi maisha ya kuvizia ili asionekane na
viongozi wa Chadema pindi akitaka kutimiziwa mahitaji ya jamii kwenye Serikali
kwani alikuwa anaonekana kama msaliti
"Ili kuonana na kiongozi wa serikali ilinipasa kuvizia, lengo
likiwa nitimize mahitaji ya wapiga kura wangu, nikajiuliza nateseka hivi kwa
ajili ya nini?" Alihoji Tlaghasi.
Amesema dhamira yake ikamtuma kuachana na Chadema na kujiunga na
CCM ili aungane na Rais John Magufuli na mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti
katika kuwatumikia wananchi.
400 kutoka chadema wahamia CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment