Kampala. Rais John Magufuli leo
amewasili nchini Uganda, kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki, unaofanyika mjini Kampala.
Katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Entebbe, Rais Magufuli amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uganda, Sam Kutesa na kisha kuelekea Ikulu ya Entebbe.
Baada ya kuwasili Ikulu amekutana
na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Pia kesho atahudhuria mkutano
maalum katika ngazi ya wakuu wa nchi unaohusu masuala ya miundombinu na afya
na keshokutwa atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki
|
Rais Magufuli awasili Uganda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment