Mwenyekiti wa CHADEMA,
Kanda ya Nyasa, Mch. Peter Msigwa amewataka waombolezaji waliofika kwenye msiba
wa Kiongozi wa chama hicho Kata ya Hananasif Kinondoni, Danie John kutokata
tamaa na kuwaambia hakuna mtu atakayeishi milele duniani.
Mchungaji Msigwa amesema hayo leo
ambapo amewaomba waombolezaji kutokata tamaa na kuendelea kupigania haki ya
kidemokrasia ambayo John ameipigania hadi mwisho wa maisha yake.
Aidha Msigwa amesema kwamba kifo cha
John kimetokana na shughuli zake za kisiasa lakini hali hiyo isiwakatishe tamaa
katika kupambania demokrasia.
Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar, Salum Mwalimu amepoteza maisha akipigania haki ya kidemokrasia.
"Tunaamini John amefariki
akitimiza majukumu yake ya kupiga kampeni kutafuta kura kwa ajili yangu na
chama chake akipendacho,"
Aidha Mwalimu amesema kwamba endapo
utamaduni wa miili ya watu kuokotwa ufu kweni ukichwa utaandaa kizazi
kitakacholipa kisasi.
John alikuwa Katibu wa Chadema, Kata
ya Hananasif, Kinondoni, Dar es salaam na mwili wake uliokotwa ufukweni mwa
bahari ya hindi ambapo ulikuwa na majeraha ya kupihwa na kitu baada ya kutoweka
Februari 11.
Msigwa awapa maneno mazito waombolezaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment