Msanii wa filamu nchini
Irene Uwoya amefunguka na kudai kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya
kuwakatisha tamaa wenzao katika vitu ambavyo wanavifanya na kupelekea wanaume
ndio wanawapa ushirikiano kwenye masuala yao jambo ambalo sio zuri.
Uwoya ameeleza hayo kupitia ukurasa
wake wa kijamii baada ya kuwepo tabia hiyo kwa muda mrefu katika jamii, ofisini
na sehemu nyingine.
"Hivi kwanini wanawake tunakuwa
hatupendani, yani najiulizaga sanaaa badala sisi tushirikiane ndio kwanza
tunarudishana nyuma. Mtu akifanya kitu kizuri au biashara ndio wa kwanza
kuponda na kurudishana nyuma",
amesema Uwoya.
Pamoja na hayo, Uwoya
ameendelea kwa kusema "yani unamskia mtu kabisa anakuponda mbaya halafu
hujawahi hata kugombana nae na pengine unamsaidiaga tu sana. Yani unashanga
wanaokuunga mkono ni wanaume badala ya wanawake wenzako, halafu ukifanya mabaya
ndio anakusifia balaaah ili uwendele kuharibu".
Aidha, Uwoya amesema kwamba pindi
ikitokea kwa watu wa aina hiyo wameanzisha biashara yake basi yeye ndio huwa
anapenda kuungwa mkono huku akijisahau kwamba yeye hakuwahi kuwasaidia wenzake
katika masuala hayo
"Nimeamua sasa hivi
nisi-support mtu yeyote asie ni-support na haina haja ya kuleana kabisa mtu
asie kuwa na umuhimu kwenye maisha yako haina haja ya kuwa sehemu ya maisha
yako atakurudisha nyuma tu. Achana na watu wasio na faida wala mchango wowote
kwenye maisha yako", amesisitiza
Uwoya.
Kwa upande mwingine, Uwoya
amewashauri wanawake wenzake na jamii kwa ujumla kutokuwa na marafiki ambae
muda wote anakushauri kufanya starehe badala ya kukupa fikra za kutengeneza
biashara ili uweze kupata fedha.
"wanawake wamekuwa na tabia ya kuwakatisha tamaa wenzao- Uwoya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment