Mkuu wa wilaya ya
Pangani Bi. Zainab Abdallah, ameushangaza umma baada ya kumpongeza mume wake
kwa kuongeza mke wa pili, kwani ni kitendo cha nadra sana kwa wanawake kufanya
hivyo licha ya kuwa misingi ya dini inaruhusu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram
mkuu wa wilaya huyo ameandika ujumbe huku akiujulisha umma kuwa wazo la mume
wake kuongeza mke wa pili lilitoka kwake, baada ya kuona majukumu ya kazi
yanambana na kushindwa kutekeleza majukumu ya ndoa.
“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi
hii kumpongeza Mume wangu kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini
yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na
uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo
mume wangu kukosa huduma za msingi”, ameandika Bi. Zainab Abdallah.
Mheshimiwa huyo wa serikali ya wamu
ya tano aliendelea kuandika kuwa ...”Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi
ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya
ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa
kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa
rabb atupe stara inshaaAllah.
Mkuu wa wilaya ampongeza mumewe kwa kuongeza mke
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 21, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment