Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwene amemsimamisha kazi Mhandisi Goyagoya Mbena
kwa tuhuma za kusaini barua ya kuruhusu ujenzi wa mradi wa Maji wilayani Nkasi
mkoani Rukwa.
Taarifa iliyotolewa leo na Wizara
hiyo, imeeleza kuwa Mhandisi Mbena amesaini barua kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
wizara hiyo kinyume cha utaratibu hivyo Waziri Kamwene amemwagiza katibu
kumsimamisha kazi mara moja ili kupisha uchunguzi.
Mradi huo wa Maji katika kijiji cha
Kamwanda Halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa umeelezwa kuwa na thamani ya
shilingi bilioni 7.4.
Waziri amsimamisha Mhandisi Kwa kusaini barua kinyume cha Utaratibu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment