Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA, kimechukua hatua ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kitendo cha kuwasamehe wafungwa
wakiwemo Babu Seya na mwane Papii Kocha.
Kwenye Taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari, chama hiko kimesema ni kitendo cha ujasiri kwa Rais Magufuli
kuendelea kutekeleza ahadi ambazo zilitolewa na chama hiko wakati wa kampeni
zake mwaka 2015.
Sambamba na pongezi hizo, CHADEMA
pia kimeomba serikali kutumia mamlaka iliyonayo kufuta kesi za mashehe wa
Zanzibar ambao kesi yao iko mahakamani, pamoja na watu mbali mbali wenye kesi
za makosa ya kimtandao.
Isome hapa taarifa yote
CHADEMA yampongeza Raisi Magufuli kwa kufanya kitendo cha ajasiri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment