Mkuu wa Gereza Dar Babu Sea atakuwa Nje Leo

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mboje amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha taratibu za kumtoa gerezani Nguza Viking na mwanaye Papii Kocha

Mboje amesema hayo baada ya Rais John Magufuli kuwasamehe wafungwa hao ikiwa ni miaka 56 ya uhuru wa Tanzania

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo Jumamosi jioni, Mboje amesema sasa hivi wanajaza fomu na itakapofika saa  11 watawaachia wafungwa hao

Tarari ndugu jamaa na marafiki wa wanamuziki hao wako nje ya gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam wakiwasubiria


Ndugu hao ambao wameonekana wakiwa kwenye magari huku wengine wakizunguka zunguka nje ya gereza hilo kusubiria taratibu za wanamuziki hao kukamilika ili waachiwe
Mkuu wa Gereza Dar Babu Sea atakuwa Nje Leo Mkuu wa Gereza Dar  Babu Sea atakuwa  Nje Leo Reviewed by KUSAGANEWS on December 09, 2017 Rating: 5

No comments: