Msanii wa muziki wa
kizazi kipya ambaye ni rafiki kipenzi wa Papii Kocha mfalme mtoto wa Babu Seya,
Bushoke Rutta, ameelezea furaha yake baada ya kusikia rafiki yake huyo
ameachiwa kwa msamaha wa Rais, na kwamba ametimiza ndoto zao.
Akizungumza, Bushoke amesema furaha
aliyonayo hailezeki kwa alichokifanya Rais na haoni wa kuchukua nafasi yake,
kwani alichokifanya ni kitendo cha huruma na upendo wa hali ya juu,
kwa kutimiza tumaini ambalo walikuwa nalo rafiki zake hao vipenzi.
Bushoke ameendeleea kusema kwamba
hivi karibuni rafiki yake huyo alimsikia akisema ana imani Rais wa sasa
atawaonea huruma na kuwaacha huru, hata isingekuwa leo basi ingekuwa siku
yoyote lakini waliamini hawatafikwa na umauti wakiwa jela.
Akiendelea kusimulia furaha yake
Bushoke amesema aliposikia Rais anatangaza kumsamehe Babu Seya na familia yake,
mwili ulimsisimka huku asiamini nachokisikia.
BUSHOKE "NILIPOSIKIA RAISI AMEMSAMEHE BABU SEA MWILI WANGU ULISISIMKA"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment