Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwemo familia ya msanii
Nguza Viking.
Pamoja na pongezi hizo LHRC,
imesema itaendelea kumuomba Rais Magufuli abadili baadhi ya sheria ikiwemo
kuondoa sheria inayotoa ruhusa ya adhabu ya kifo..
“Tunampongeza Mh. Rais Magufuli kwa kutoa msamaha kwa wafungwa
61 kati ya wafungwa 522 waliohukumiwa kunyongwa”. LHRC wameandika kupitia
ukurasa wao wa Twiiter.
Rais Magufuli ametoa msamaha huo leo kwenye sherehe za
maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma.
LHRC imeongeza, “Tunamsihi
Mhe. Rais kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta sheria zinazoruhusu uwepo
wa adhabu ya kifo na kuifanya hukumu ya kifungo cha maisha kuwa adhabu
mbadala”.
Katika msamaha huo Rais pia amemsamehe mzee Mganga Matonya
ambaye ana miaka 85 akiwa amekaa gerezani miaka 37 pamoja na miaka saba
aliyokaa mahabusu wakati akisubiri hukumu yake hivyo kufanya afikishe miaka 44
gerezan
LHRC WAMPONGEZA RAISI MAGUFULI KWA KUMSAMEHE BABU SEA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment