Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amemsimamisha kazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Bw. Julius Mseleche
Kaondo, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa.
Akiongea na wanahabari ofisini kwake
mjini Dodoma, Mh. Jafo amesema kuwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi huyo kutokana
na mamlaka aliyopewa chini ya kifungu Na. 4 (1-5) cha Sheria ya Serikali za
Mitaa (Mamlaka na Wilaya) sura 287 kwa mujibu wa Kanuni ya 36 ya Kanuni za
Utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Mkurugenzi huyo anatuhumiwa
kujihusisha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa zabuni ya miradi ya Maji
na kushindwa kusimamia manunuzi katika utekelezaji wa miradi ya
maji, katika kijiji cha Kamwanda Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa na
kusababisha mradi huo kutokamilika kwa wakati.
Mhe. Jafo amesema mradi huo ulikuwa
ukigharimu shilingi bilioni 7 na wenye lengo la kutatua kero ya Maji
katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi na kuwaletea maendeleeo wananchi wa
wilaya hiyo.
Aidha Waziri Jafo ametoa wito kwa
Wakurugenzi , Wakuu wa Idara, pamoja na watumishi wa Mamlaka za Serikali za
Mitaa nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo.kwa kushindwa kusimamia hatua
za manunuzi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Nkasi atumbuliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment