Wapalestina wamezima taa za krismasi
kwenye mji mtakatifu wa Bethlehem alikozaliwa Bwana Yesu, kupinga hatua ya Rais
wa Marekani Donald Trump ya kuutambua mji wa Yerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Afisa Habari wa Manispaa ya
Bethelehem, Fady Ghattas amesema Mti wa Krismasi ulioko kwenye kanisa la
Bethlehem ambako wakristo huamini Bwana Yesu alizaliwa, ulizimwa taa zake kwa
amri ya Meya wa Manispaa hiyo.
Miji mingine iliyozimwa taa ni
Ramallah ulio karibu na mahali alipozikwa kiongozi wa zamani wa Palestina
Yasser Arafat.
Waarabu na waislamu katika nchi za
Mashariki ya kati wamepinga hatua ya Trump ya kutangaza kutambua Yerusalem kuwa
mji mkuu wa Israel.
Wapalestina wazima taa za Krismasi mjini Bethlehem kupinga tangazo la Trump
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment