Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameagiza utekelezaji wa
Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira uwe ni ajenda ya kudumu ya kila ngazi ya
Uongozi.
Makamu wa Rais ameyasema hayol eo
wakati wa Uzinduzi wa Kamapeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya Pili
ukiofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang’ombe,mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais alisema Serikali
imejiwekea mikakati mbali mbali ya kupambana na maradhi ya kuambukiza ambapo
usafi wa mazingira ni njia mojawapo ambapo katika awamu ya kwanza ya kampeni ya
Taifa ya Usafi wa Mazingira ambapo jumla ya kaya 1,662,550 zilijengwa vyoo na
shule 2,133 vilijengwa vyoo bora.
Katika awamu ya Pili iliyozinduliwa
leo kaya 5,600,000 zinatarajiwa kuongeza idadi ya vyoo bora na shule za
msingi 3,500 na sekondari 700 zitapata huduma ya vyoo bora na sehemu maalum ya
kunawa mikono baada ya kutoka chooni.
“Wahenga walisema Samaki
mkunje angali mbichi, methali hii inatukumbusha jukumu la kuwafundisha watoto
wetu umuhimu wa usafi wa mazingira tangia wadogo wakiwa mashuleni”alisisitiza
Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais alitoa Wito kwa
Wanawake wote nchini kujifunga Kibwebwe na kujenga vyoo, alisema Wanawake
wamekuwa na vikundi mbali mbali vya kusaidiana na kuwezeshana hivyo kwa kupitia
vikundi hivyo wanaweza kufanikisha ujenzi wa vyoo bora majumbani.
Makamu wa Rais aliwapongeza Washindi
wote wa Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2016/17. Pia aliwashukuru wadau
mbali mbali ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine kufanikisha
uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira.
Makamu wa Rais azindua rasmi kampeni ya Kitaifa ya usafi awamu ya pili,Dodoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment