Nchi ya Marekani imemtaka Kiongozi
Mkuu wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama
rais wa nchi hiyo wiki ijayo Desemba 12, 2017.
Msaidizi wa Katibu wa Masuala ya
Afrika Marekani, Donald Yamamoto alipotembelea Kenya, ametaka kuwepo
majadiliano ya pande zote mbili baina ya upinzani na serikali iliyoko
madarakani.
Licha ya wito huo, baadhi ya
viongozi wa serikali wameonya kwamba tukio hilo la kuapishwa Odinga, linaweza
kuhusishwa na kosa la uhaini.
Odinga baada ya uchaguzi Mkuu wa
Kenya kufanyika alitoa malalamiko kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwenye
uchaguzi huo na kupelekea uchaguzi kurudiwa ambapo Uhuru Kenyata alishinda kwa
kishindo.
Chanzo: BBC
Marekani yamtaka Odinga kusitisha mpango wa kuapishwa kuwa Rais
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment