Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dk John Pombe Magufuli ametaka
kuvunjwa kwa bodi ya wadhamini ya umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi
UVCCM na kuwataka viongozi watakaochaguliwa kuhakiki miradi yote ya umoja huo
kuanzia ngazi ya chini.
|
Akifungua mkutano wa tisa wa
jumuia hiyo ambao ajenda yake kuu ni kufanya uchaguzi wa viongozi Rais
Magufuli amesema kuwa miradi ya UVCCM mapato yake yamekuwa hayajulikani
yanapoenda hivyo inahitaji kuhakikiwa na kuwekwa pamoja ili kuweza kuleta
tija kwa umoja huo huku akisema bodi ya wadhamini imekuwa haina msaanda
katika jumuia hiyo.
|
Rais Magufuli pia amewataka UVCCM
kuchagua viongozi wanaofaa na wanaoichukia rushwa ili waweze kuisaidia
serikali badala ya kuwa viongozi wa kuyumbishwa na misimamo ya watu wenye
pesa hali iliyofanya umoja huo kukosa muelekeo hasa kipindi cha uchanguzi
|
Katika mkutano huo wanachama wapya
waliojiunga na chama hicho hivi karibuni kutoka vyama mbalimbali waliwataka
vijana wa CCM kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali.
|
Katika hatua nyingine Rais
Magufuli amesema Mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake Sadifa Juma Hamisi
anashikiliwa na Tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kwa tuhuma
za kujihusisha na vitendo vya rushwa
|
Magufuli " Bodi ya wadhamini UVCCM ivunjwa"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment