Mwenyekiti wa (CCM)
Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wajumbe wa Umoja wa Vijana wa chama hicho
(UVCCM) kuwa endapo watachagua viongozi kama waliokuwepo awali watambue
watapata shida kwa miaka mingine mitano.
Magufuli amesema hayo leo Disemba
10, 2017 akiwa Makao Makauu ya nchi mjini Dodoma alipohudhuria Mkutano Mkuu wa
tisa wa UVCCM Taifa ambapo amewataka vijana wa chama hicho wasiogope kufanya
maamuzi yenye kuleta mabadiliko katika safu ya uongozi wa Umoja huo kwa kuwa
viongozi waliokuwepo tayari wameonyesha kuwa na dosari na kuwakosesha nafasi
vijana wengi kuweza kupewa nafasi katika serikali ya awamu ya tano.
"Mwenyekiti mtakaye mchagua,
Makamu Mwenyekiti na uongozi wote wa vijana mtakaouchagua leo hao ndiyo
watakuwa washauri wangu wakubwa ila mkichagua kama wale ambao hawakunishauri
hata kwa kuniletea majina ya kuteua kwenye nafasi zenu, mkachagua tena katika
mwaka huu mjue mna miaka mitano mingine ya kuumia" alisisitiza Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli aliwataka vijana
hao kutowachagua viongozi wa UVCCM ambao wanatumia fedha kutaka kupata
nafasi ndani ya umoja huo wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Awataka vijana wa chama hicho wasiogope kufanya maamuzi yenye kuleta mabadiliko " - Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment