![]() |
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies . |
![]() |
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine huko Chicago Nchini Marekani wakiwa wameshika tuzo zao. |
![]() |
Picha ya tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies iliyotolewa kwa jiji la Dar es Salaam Chicago Nchini Marekani. |
JIJI la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani
ambayo yamepata tuzo ya C40 Bloomberg Philantropies 2017
kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.
Katika tuzo hiyo mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa
jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka
huu.
Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo na Jiji la New
York nchini Marekani na .
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila
siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa
magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya
mafanikio ya tuzo jijini hapa.
Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka
katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua
jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90
duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya
Tabia ya Nchi Duniani.
Kaption.
Px. 1 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa
neno la shukrani baada ya kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies .
Px. 2 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa
kwanza kushoto mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine
huko Chicago Nchini Marekani wakiwa wameshika tuzo zao.
Px 4 Picha ya tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies iliyotolewa
kwa jiji la Dar es Salaam Chicago Nchini Marekani.
Imetolewa leo Desemba 10
Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa
jiji.
Jiji la Dar es Salaam lapata tuzo kupitia Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment