Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa umeme
kwa njia ya luku na kusema kuwa kwa sasa upo sawa na wanaweza kununua katika
mifumo iliyozoeleka.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam Kaimu Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano(TEHAMA) wa Tanesco, Demetruce
Dashin amesema kuwa kulitokea tatizo dogo la mfumo wa ununuzi wa umeme kwa
njia ya Luku kutokana na wataalamu wa shirika hilo walipokuwa wakiamisha
mitambo hiyo kutoka ofisi ya Zamani kwenda sehemu nyingine.
Bw. Dashina amefafanua kwamba
kufuatia taharuki ya tatizo la kimtandao lililotokea jana kupelekea watu kupata
shida katika ununuzi wa umeme Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limesema tatizo
la kimtandao ambalo lilianza jana kufuatia hitilafu katika mfumo
limeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo wanatarajia kumaliza tatizo hilo
ndani ya siku chache.
“Jana tulikuwa tunafanya uhamisho wa
mfumo wa luku kwende katika ofisi zetu mpya hivyo ikawalazimu wateja wetu
kupata usumbufu kidogo, lakini kuanzia saa saba mfumo huo umekaa sawa na wateja
wanaweza kununua umeme kama walivyokuwa wanafanya hapo awali bila shida yoyote
mara baada ya marekebisho ya kiufundi” amesema Dashina
Aidha Bwana Dashina amesema mpaka
sasa wataalamu wanaendelea na zoezi la ukarabati ambalo limekamilika kwa
asilimia kubwa ambapo wanaendelea na uhamishaji mitambo kutoka ofisi zao za
zamani na kuweka kwenye ofisi mpya.
Kwa upande wake Kaimu
Meneja Uhusiano wa Tanesco Leila Muhaji amewaomba radhi wananchi kwa
usumbufu uliojitokeza na kuwasisitiza kuwa sasa wanaweza kununua katika mifumo
iliyozoeleka.
Muhaji amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo kuwataka watanzania kuwa na imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia kama inavyohitajika na kuongeza kwamba tukio hilo la jana limesimamisha shughuli nyingi ambazo zimerudisha nyuma shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuwahakikishia wananchi tatizo hilo kumalizika haraka iwezekanavyo.
Muhaji amesema kuwa Tanesco inatambua umuhimu wa umeme hivyo kuwataka watanzania kuwa na imani na shirika lao kwani lipo kwa ajili ya kuwahudumia kama inavyohitajika na kuongeza kwamba tukio hilo la jana limesimamisha shughuli nyingi ambazo zimerudisha nyuma shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kuwahakikishia wananchi tatizo hilo kumalizika haraka iwezekanavyo.
TANESCO yaomba radhi wateja wake.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 10, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment