Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimeazimia kuwa wabunge wake wote wanaoshiriki Michezo ya Mabunge ya
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatakiwa kuondoka mara moja kwenye
kambi ya timu ya Tanzania.
CHADEMA kimefikia uamuzi huo katika
kikao chake cha dharura kinachoendelea ambacho kiliitishwa kwa lengo la
kutafakari kwa kina maendeleo ya hali ya siasa nchini.
Chama hicho kimesema kuwa maagizo
hayo yameanza kutekelezwa usiku wa Jumatano, Disemba 6 mwaka huu baada ya
kupitishwa kwa azimio hilo ambapo Kamati Kuu ilimuagiza Katibu wa Bunge kuwafikishia
wabunge wahusika mara moja
Baada ya kupokea tathmini ya kina ya
Uchaguzi wa marudio katika Kata 43 uliofanyika hivi karibuni CHADEMA kimebaini
kuwa ulitawaliwa na uvunjifu Mkubwa wa Haki za binadamu.
Aidha CHADEMA kimesema kuwa maazimio
mengine ya kikao cha Kamati Kuu ambacho kinaendelea jijini Dar yatatolewa
katika hatua ya baadae ambapo umma utaarifiwa rasmi.
CHADEMA chawataka wabunge wake kujiondoa michuano ya mabunge EAC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 07, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment