Baada ya Rais Magufuli
kutoa msamaha kwa familia ya Nguza Viking na wafungwa wengine leo, tayari Nguza
Viking na mwanae Johnson Nguza wametoka katika gerezani la Ukonga jioni hii.
Nguza na wanawe watatu walikamatwa
Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar,
walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka
2003 wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10.
Baada ya kusikilizwa kesi hiyo Juni
25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy
Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwenda jela maisha kwenye Gereza
la Ukonga, Dar es Salaam.
Mwaka 2010 waliomba rufaa ambayo
marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari, 2010. Mahakama
iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha, ikawaachia
huru watoto wake, Mbangu na Francis Nguza.
Rais Magufuli leo akiwa kwenye
sherehe za Uhuru jijini Dodoma alitangaza kuisamehe familia hiyo pamoja na
wafungwa wengine 8,157 ambapo 1828 watatoka leo huku 6329 wakipunguziwa muda wa
kukaa gerezani.
BABU SEA NA MWANAE TAYARI WAKO HURU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

1 comment:
God bless our President!
Post a Comment