Hatua ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya ya kujiapisha
imepata pigo baada ya mwanasheria mkuu Githu Muigai kusema kuwa hatua hiyo ni
uhaini na hukumu yake ni kifungo cha maisha jela.
Hatua ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya ya kujiapisha imepata
pigo baada ya mwanasheria mkuu Githu Muigai kusema kuwa hatua hiyo ni uhaini na
hukumu yake ni kifungo cha maisha.
Akizungumza na wanahabari Muigai amesema hatua
ya mabunge ya majimbo kupitisha miswada ya kuanzisha vikao vya mabunge ya
wananchi pia ni kinyume cha sheria.
Aidha marekani imemtaka Odinga kutojiapisha ikisema ni ukiukwaji
wa sheria. Wakati huo huo Odinga ameilani vikali jamii ya kimataifa kwa
kunyamazia ukiukaji wa haki za binadamu baada ya uchaguzi mkuu uliotekelezwa na
maafisa wa polisi.
Tamko la mwanasheria mkuu Githu Muigai linajiri siku nne kabla
ya kiongozi wa upinzani raila Odinga kujiapisha kwa kutumia mabunge ya majimbo.
Tayari majimbo 12 yamepitisha mswada wa kujenga vikao vya
mabunge ya wananchi ambayo hayatambui uhalali wa rais Kenyatta. Kama ishara
ambayo serikali ya rais Uhuru Kenyatta haitavumilia hatua ya Odinga, Muigai
alisema.
Kenya: Mwanasheria mkuu amkosoa Raila kwa kutaka kujiapisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment