Mkuu wa Mkoa wa
Manyara mstaafu, Joel Bendera amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH).
Msemaji wa MNH,
Aminiel Aligaesha amesema, “Ni kweli Joel Bendera amefariki. Aliletwa leo na
gari la wagonjwa saa 6:30 mchana na ilipofika saa 10:24 jioni alifariki.”
Aligaesha amesema
Bendera alipokewa hospitalini hapo akitokea Bagamoyo mkoani Pwani.
Kuhusu chanzo cha kifo
chake Aligaesha amesema, ‘’Hilo sasa ni suala la familia lakini kwa wakati huu
itoshe kusema amefariki.”
Bendera pia amewahi
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Mbali ya ukuu wa mkoa,
amewahi kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na
Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Katika mabadiliko ya
wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli Oktoba 26,2017, Bendera
alikuwa miongoni mwa waliostaafu.
Nafasi yake
imechukuliwa na Alexander Mnyeti aliyepandishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara
akitokea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara afariki dunia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 06, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment