Mbunge Ester Bulaya akamatwa na polisi

Mbunge wa Bunda Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Ester Bulaya amekamatwa na jeshi la Polisi wilayani Tarime na kwenda kufanyiwa mahojiano na polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya kwa kile kilichoelezwa kufanya mkutano nje ya jimbo lake.

Akizungumza Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema kuwa mbunge huyo amekamatwa na jeshi la polisi kwa kushiriki kwenye mkutano wa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini John Heche uliofanyika jana.

Amesema Ester amekamatwa na kufikishwa polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya,na polisi wamedai kuwa walikuwa wanamtafuta baada ya yeye kushiriki kwenye mkutano wa hadhara ambao ulifanyika Nyamongo, kwenye jimbo la la Tarime vijijini ambapo Mbunge John Heche alikuwa na ziara ya jimbo.

Mbunge Ester Bulaya wiki hii alikuwa na ziara pia katika jimbo lake kusikiliza maoni mbalimbali ya watu na kuwashukuru wananchi wake kwa kuwa wavumilivu kwa muda mrefu kufuatia kesi mbalimbali ambazo zilikuwa zikimuandama kutokana na Mbunge wa zamani wa jimbo hilo kufungua kesi kadhaa mahakamani kupinga ushindi wa Ester Bulaya


Mbunge Ester Bulaya akamatwa na polisi Mbunge Ester Bulaya akamatwa na polisi Reviewed by KUSAGANEWS on August 19, 2017 Rating: 5

No comments: