Rais wa (TLS), Tundu Lissu amefunguka na kusema wabobezi
wa sheria nchini akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja
na Waziri wa Katiba Na Sheria Prof Palamagamba Kabudi wanamsikitisha kwa kuwa
wanashindwa kuishauri vizuri serikali
"Bungeni kulijitokeza mjadala na
nikazungumza lakini Dr Mwakyembe na Profesa Kabudi walinijibu kuwa sisi kama
nchi huru hatuwezi kuogopa kushtakiwa katika mahakama ya Kimataifa kwa kuvunja
mikatba na kuvunja wajibu wetu kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa mujibu wa mikataba
ya kimataifa tulioisaini na ambayo sisi ni wanachama. Nisema hapa kwa masikitiko
makubwa kabisaa wanasheria waliobobea ambao wanatakiwa kumuelekeza Mhe. Rais
sawa sawa wamekuwa hawatekelezi wajibu wao kwa sababu pengine ya kuogopa
kutumbuliwa au kwa sababu zingine ambazo zipo kinyume na taaluma zao kabisa
moja wapo wa ushauri wa namna hii ni hizi kauli kwamba hatutakiwi kuogopa
kushtakiwa katika mahakama za kimataifa ni ushauri ambao ukitoka kwa
mwanasheria unasikitika kabisaa" alisema Tundu
Lissu
Wanaogopa kutumbuliwa - Tundu Lissu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment