ZAIDI YA KAYA ELFU 50 KATIKA VIJIJI SITA WILAYANI ARUMERU KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA




Zaidi ya kaya elfu hamsini katika vijiji sita vya wilaya ya Arumeru zinatarajia kunufaika na mradi wa maji safi na salama utakao endeshwa kwa kiteknolojia mpya ya kulipa kwa kadiri wanavyotumia kama ilivyo kwa umeme wa luku ambao unatajwa kumaliza tatizo sugu la maji kwenye eneo hilo mradi unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni nne.

Wakizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo uliyofadhiliwa na serekali ya Uingereza kupitia mpango wake wa kusaidia maeneo yenye umasikini uliotopea,wakazi wa vijiji hivyo pamoja na wawakilishi wa wananchi wamesema utakuwa mkombozi kwa wananchi ambao wameteseka na kero ya maji  kwa muda mrefu.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Dakta WILSON MAHERA amesema halmshauri itahakikisha mradi huo unalindwaipasavyo huku akitoa onyo kwa watendaji watakaosimamia mradi huo kutoingiza siasa na zulma kwa wananchi.

Naye Mkurugenzi wa shirika linalosimamia ujenzi wa mradi huo ABEL DUGANGE amesema lengo la mradi huo ni kumaliza kero ya maji kwenye eneo hilo lakini shirika limeamua kuendesha kwa teknolojia ya kulipa kadiri wanavyo tumia,ili kuondoa uwezekano wa kufanyika kwa ubadhilifu wa fedha na kuhujumu mradi.


ZAIDI YA KAYA ELFU 50 KATIKA VIJIJI SITA WILAYANI ARUMERU KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA ZAIDI YA KAYA ELFU 50 KATIKA VIJIJI SITA WILAYANI ARUMERU KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA Reviewed by KUSAGANEWS on July 09, 2017 Rating: 5

No comments: