Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge ameagiza kupitiwa upya kwa mkataba wa ujenzi wa bomba la mradi wa maji katika wilaya ya Bunda mkoani Mara kutoka katika chanzo cha maji cha Nyabehu kwani haridhishwi na utendaji kazi.
Mh. Lwenge ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea mradi huo ambao ulianza ujenzi wake tangu mwaka 2011 kupitia kampuni ya ujenzi ya Nyakirang'anyi ya mkoani humo ambapo amesema hafurahishwi na ujenzi wa kampuni hiyo katika miradi mbalimbali ya maji inayopewa.
Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Esther Bulaya amepongeza uamuzi wa Waziri na kusema;
"Tatizo la maji katika mji wa Bunda limekuwa sugu kwa kauli hii ya waziri kutaka kupitia upya mikataba ya ujenzi huu inatia matumani", Bulaya
No comments:
Post a Comment