Kiwanda cha kutengeneza magunia ya katani kilichoanza
uzalishaji wake mwaka 1998 mkoani Morogoro (TPCM) kimefungwa na kusitisha
uzalishaji tangu April 2016 kufuatia kukosa soko la bidhaa hiyo hatua ambayo
imetajwa kusababishwa na uingizwaji wa mifuko ya viroba kutoka nje ya nchi huku
ajira za wafanyakazi 900 wa kiwanda hicho zikisitishwa.
Kufungwa kwa kiwanda hicho kumebainika wakati wa ziara ya
Mkuu wa mkoa huo Kebwe Steven Kebwe ya kukagua hatua walizofikia wamiliki wa
viwanda katika kufufua na kuanza uzalishaji
Katika hatua nyingine kilichokuwa kiwanda cha kuzalisha
mafuta ya kula yanayotokana na mbegu za alizeti cha Moprock kimeanza uzalishaji
baada ya kusitisha uzalishaji huo kwa zaidi ya miaka minane iliyopita,huku
kikitarajia kumaliza tatizo la ukosefu wa soko la alizeti kwa wakulima wa mikoa
ya Morogoro,Dodoma pamoja na Singida
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa mkoa wa Morogoro
Dokta Kebwe amemuagiza Mkurugenzi wa Moprock kumalizia ukarabati uliobaki ili
uzalishaji uendelee huku akieleza kusikitishwa na hatua ya kiwanda cha magunia
kusitisha uzalishaji
KIWANDA CHA KUTENGENEZA MAGUNIA YA KATANI MOROGORO CHAFUNGWA KWA KUKOSA SOKO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment